Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bao tano za Yanga zimetupa morali - Ahmed Ally

Ahmed Ally Bao 5 Bao tano za Yanga zimetupa morali - Ahmed Ally

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Simba imesema kitendo cha kufungwa bao 5-1 na wapinzani wao, Yanga SC kumewapa morali ya kupambana zaidi ili kupata alama tatu katika kila mchezo unaokuja mbele yao.

Ahmed amesema hayo kuelekea mchezo wa leo wa Ligi ya Kuu ya NBC dhidi ya Namungo katika Dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam huku akitamba kuwa mchezo huo wataondoka na alama tatu.

"Hali ndani ya kikosi cha Simba iko shwari, baada ya dhoruba tumerejea kwenye maisha yetu na mambo yanakwenda vizuri.

"Baada ya kupoteza mchezo wetu dhidi ya Yanga uongozi unafanya tathmini na hatua zimeshaanza kuchukuliwa kwa kuwaondoa makocha wetu, Robertingo na mwenzake wa viungo Hategekimana Corneille. Tunaendelea kufanya tathmini kujua wapi tumekosea kwenye mchezo huo ili tufanye maboresho zaidi.

"Sasa hivi tumeshaachana na mawazo ya mechi iliyopita, akili yetu ni kuelekea mchezo unaofuata wa Ligi dhidi ya Namungo na ule dhidi ya Azam FC. Hili ndilo la muhimu zaidi kwa sasa. Haiwezi kufuta machungu kwa kufungwa na mtani wako namba moja.

"Matokeo tuliyoyapoteza Jumapili hatuwezi kuyarudisha tena, hata ukilia vipi huwezi kumfufua maiti wako. Kwa hiyo hata tukilalamika vipi hatuwezi kurejesha alama tatu tulizopoteza, cha kufanya ni kuangalia namna ya kuchukua alama tatu kwa Namungo na Azam FC badala kufikiria tulizopoteza.

"Simba hatufanani na hao ambao walifungwa na namungo au aliwakazia, tunajua namna ya kumalizana na hawa wadogo wadogo, matokeo tulioyapata Jumapili yanatupa morali ya kupambana kupata alama tatu. Heshima ya Mnyama itarejea kesho (leo) katika Dimba la Uhuru," amesema Ahmed Ally.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live