Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bao la jioni lafanya Ronaldo akere watu

Bao La Jioni Bao la jioni lafanya Ronaldo akere watu

Thu, 20 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Supastaa, Cristiano Ronaldo amekosolewa na mashabiki kwa namna alivyoshangilia ushindi wa dakika za mwisho iliyopata Ureno kwenye mchezo wao wa kwanza wa fainali za Euro 2024 dhidi ya Jamhuri ya Czech juzi Jumanne.

Kikosi hicho cha Ureno chini ya kocha Roberto Martinez kilitokea nyuma kwenye mchezo huo na kushinda 2-1 huko jijini Leipzig.

Lukas Provod aliifungia Czech bao la kuongoza kwenye dakika ya 62, lakini, Ureno ilipindua mechi. Bao la kujifunga la mchezaji, Robin Hranaj liliifanya Ureno kusawazisha na ubao wa matokeo kusomeka 1-1 wakati mechi ikiwa imebakiza dakika 20 za mwisho.

Ureno ilifunga bao lingine kupitia kwa Diogo Jota, lakini lilikataliwa, kabla mtokea benchini Pedro Neto kumpigia pasi matata kabisa mtokea benchini mwenzake, Francisco Conceicao na kufunga bao la ushindi kwenye dakika ya 92.

Bao hilo la dakika za mwisho liliwavuruga Ureno kwa furaha, ndipo supastaa Ronaldo alipokwenda kushangilia mbele ya kipa wa Czech, Jindrich Stanek, kitendo ambacho kimewakasirisha mashabiki na kumsema staa anayekipiga Al Nassr. Shabiki mmoja aliandika kwenye mtandao wa kijamii: “Hakupaswa kufanya vile. Sio kitu kizuri.”

Shabiki wa pia aliandika: “Ni ngumu kushangilia timu isiyokuwa na heshima na wachezaji wa hovyo wenye majina makubwa kama hawa.”

Shabiki wa tatu alisema: “Vitu ambavyo huoni Messi akifanya.” Na shabiki wa nne alisema: “Hovyo kabisa.”

Shabiki wa mwisho alisema: “Kila kitu kimejionyesha.”

Baada ya mechi, Bruno Fernandes alizungumzia umuhimu wa Ronaldo kwenye kikosi cha Ureno, akisema: “Sote tunafahamu umuhimu wa kuwa na wachezaji wenye uzoefu kama Cristiano Ronaldo. Kuna Pepe, mchezaji mwenye uzoefu zaidi. Tufahamu umuhimu wao kwetu.”

Ureno itashuka uwanjani Jumamosi kwa kukipiga na Uturuki huko Dortmund.

Chanzo: Mwanaspoti