Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bao la Ushindi Laondoka na Uahi wa Kocha

NINTCHDBPICT000697975538 Simanzj

Sun, 5 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya El Magd, Adham El-Selhadar amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 53 wakati akisherehekea goli la ushindi dakika ya 92 kabla mpira kumalizika kwenye ushindi wa 1 – 0 dhidi ya timu ya El Zarqa.

Adham El-Selhadar kocha wa klabu ya El Magd inayoshiriki ligi daraja la pili amefariki dunia kutokana na ‘heart attack’ alipokuwa akishangilia goli hilo pekee na la ushindi siku ya Alhamisi.

Ghafla hali yake ilibadilika na kukimbizwa hospitali baada ya kupata ‘heart attack’ wakati akiwa katika sherehe hiyo ya kushangilia bao hilo la dakika za lala sama.

Klabu za Al Ahly SC na Ismaily SC ambazo zimewahi kutumikiwa na kocha El Selhadar zimeandika ujumbe wao wa pole kufuatia kupoteza kwake maisha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live