Bao kali alilofunga Cristiano Ronaldo limevunja rekodi kwenye klabu yake ya Al Nassr na limewaacha mashabiki wakipigwa na butwaa.
Bao hilo la ushindi alilolifunga juzi Ijumaa usiku wakati Al Nassr ikicheza na Al-Akhdoud na kuichapa mabao 3-0 kwenye Ligi Kuu ya Saudia, lilikuwa la pili na mashabiki wengi waliofika uwanjani kushuhudia mchezo huo walibaki wakishangaa ufundi wa mshindi huyo mara tano wa Ballon d’Or.
Bao hilo lililowaacha mashabiki midomo wazi linatajwa na ni bao bora kwenye historia ya klabu hiyo.
Bao hili lilitokana baada ya kipa wa Al-Akhdoud, Paulo Vítor kutoka nje kuokoa, kabla ya mpira kumtoka na nyota huyo akauweka mpira kifuani kabla ya kupiga shuti la juu ya safu ya ulinzi na moja kwa moja likaingia wavuni ikiwa ni zaidi ya umbali wa yadi 30.
Kwenye mitandao ya kijamii na hasa X, shabiki mmoja akiandika: “Siamini bao limefungwa na GOAT.”
Shabiki mwingine akaandika: “Hii hairuhusiwi kabisa.” na shabiki wa tatu aliandika: “Sasa hilo ndilo gori bora la tuzo ya Puskas. Karibuni kwa mjadala.” Shabiki wa nne aliongeza: “Hakuna mchezaji anaweza kufanya hivyo duniani hiki ni kitu cha ajabu sana.”
Bao hili la Ronaldo limefanya kuvunja rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi katika historia ya soka, akimpita gwiji wa kimataifa wa Czech, Josef Bican aliyefunga mabao 527 wakati Ronaldo akiweka kambani mabao 864.
Katika mwaka huu 2023 Ronaldo amehusika kuchagia kupatikana kwa mabao 61.