Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bao la Guede; Mkono apewe maua yake

Mkono Guede Mkono apewe maua yake

Tue, 23 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Litazame bao la Joseph Guede namna mfungaji alivyochomoka haraka na kuvunja mtego wa kuotea (offside trap) ambao uliwekwa na safu ya ulinzi ya Simba na kufunga bao kililoihakikishia Yanga ushindi katika mechi ya jana.

Kwa uharaka wa lile tukio kama refa msaidizi asingekuwa makini angeweza kunyoosha kibendera kuashiria kuwa Joseph Guede ameotea lakini ilikuwa tofauti kwa refa msaidizi wa kimataifa wa Tanzania, Mohammed Mkono kutoka Tanga ambaye alitazama vizuri tukio na kugundua kuwa Guede hakuotea akatambaa na chaki, refa wa kati akaita kati.

Mechi kubwa kama ile inahitaji umakini mkubwa kama ule wa Mohammed Mkono ambaye pia ni mwalimu mkuu wa shule ya sekondari huko Korogwe ili kuepuka kumnyima mtu haki aliyostahili au kumpa mtu asichostahili.

Ahmed Arajiga anaweza kupata sifa nyingi kama mwamuzi wa kati ambaye ndiye boss wa mchezo lakini wasaidizi wake pia walichangia kwa kiasi kikubwa kumlinda kwa kumsaidia kufanya uamuzi sahihi kama alivyofanya @mkonomohamedy refa aliyechezesha Afcon U17 mwaka 2019 hapa nchini.

Timu zilitupa mechi bora ya Derby katika dakika 90 lakini pia waamuzi walijitahidi kutupa uamuzi mzuri ambao ninnadra kutokea mara kwa mara kwenye soka letu siku za hivi karibuni.

Big up Mwalimu Mohammed Mkono na wenzako. Mmejitahidi kuimaliza Derby salama. Kama ambavyo nimekuwa nawakosoa mkifanya vibaya, ndivyo ninavyowasifia kwa kufanya vizuri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live