Bao la kiungo, Abdoulaye Doucoure dakika ya 57 limeipa tena timu ya Everton matumaini ya kucheza Ligi Kuu England msimu ujao wa 2023/24 baada ya kuponea kwenye tundu la sindano kushuka daraja.
Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bournemouth uliinusuru Everton kushuka daraja baada ya Leicester City kuifunga West Ham United mabao 2-1 lakini haikufaniwa kusalia ligi kuu.
Vijana wa kocha, Sean Dyche walihitaji sana ushindi huo ili kuendelea kucheza Ligi Kuu baada ya kufikisha pointi 36, mbili zaidi ya Leicester iliyoshuka daraja ikiwa na 34 licha ya kushinda mechi yake ya mwisho baada ya ligi hiyo kufikia tamati jana Jumapili.
Timu zilizoshuka daraja ni Leicester City, Leeds United na Southampton iliyotoka sare ya mabao 4-4 dhidi ya Liverpool.
Huku Burnley ambao ni mabingwa wa Championship wakifundishwa na beki wa zamani wa Manchester City, Vincent Kompany ilikuwa ya kwanza kupanda Ligi Kuu England ikiwa na pointi 101 ikifuatiwa na Sheffield United huku Luton Town ikimalizia ukurasa huo.