Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bao la Aziz Ki, Yanga yaandika barua kwa CAF

Yanga Out CAF Bao la Aziz Ki, Yanga yaandika barua kwa CAF

Sat, 6 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Yanga SC ikiwa imepita siku moja tangu itolewe katika michuano ya CAF Champions League hatua ya robo fainali katika mchezo dhidi ya Mamelod Sundowns imeandika barua ya malalamiko kwa CAF kufuatia kukataliwa kwa goli la Azizi Ki dakika ya 57 pasipo Refa wa mchezo huo Raia wa Mauritania, Dehane Beida kwenda kujiridhisha katika VAR.

Yanga imewasilisha barua ya malalamiko kwa shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) ikituhumu upangaji wa matokeo katika mechi yao dhidi ya Mamelodi Sundowns jana ambapo ilipoteza kwa mikwaju ya penalti 3-2 baada ya dakika 90 za mchezo wa marudiano wa hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kumalizika kwa sare tasa jijini Pretoria, Afrika Kusini.

Kwenye barua hiyo ambayo Yanga imeiandika kupitia kwa Mkurugenzi wake wa sheria Simon Patrick, imewalalamikia Marefa kwa kushindwa kutumia teknolojia ya VAR kupata ufumbuzi, hivyo wanaamini na kulalamika kupitia sheria namba XVI kwamba kuna viashiria vya upangaji wa matokeo ikiwemo pia kitendo cha Refa wa kati kushindwa kwenda kwenye VAR kuangalia utata wa goli hilo licha ya kwamba aliweza kwenda kwenye VAR kuhakiki faulu ya Mchezaji wa Yanga.

Kwenye barua hiyo pamoja na mambo mengine Yanga wameiomba CAF ichunguze tukio hilo kwa undani kwa kutumia ushahidi wa rekodi za VAR na footage za mechi ili kubaini endapo kuna viashiria vya upendeleo kwa Mamelodi vimefanyika na ikijiridhisha kuna upendeleo ichukue hatua kwa kila aliyehusika, iweke hatua madhubuti za kudhibiti tukio kama hilolisijirudie kwenye mechi zijazo na pia ichukue maamuzi mengine ambayo CAF itaona yanafaa chini sheria za mpira za CAF namba XVI kifungu namba 3.

Katika mchezo huo,Yanga ilipata bao katika dakika ya 57 kupitia kwa Stephen Aziz Ki lakini lilikataliwa na mwamuzi Beida Dahane wa Mauritania kwa msaada wa marefa waliokuwa katika chumba cha teknolojia ya usaidizi wa video kwa marefa (VAR) wakidai mpira haukuvuka mstari wa goli kwa asilimia 100.

Hata hivyo picha za marudio ya luninga zinaonyesha kuwa mpira huo ulivuka wote mstari wa goli na hivyo bao la Yanga lilipaswa kukubaliwa.

"Tunaomba uchunguzi wa kina wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika kuanika viasharia vyovyote vya kosa la kiutawala na upangaji wa matokeo. Vitendo kama hivi vinaathiri ushindani wa mchezo na vinapaswa kuchukuliwa hatua ili kudumisha uaminifu wa mashindano ya Caf," ilifafanua barua hiyo ya Yanga.





Chanzo: www.tanzaniaweb.live