Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bango lajeruhi mashabiki Uholanzi

Baongo Uholanzi Bango lajeruhi mashabiki Uholanzi

Mon, 24 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wasiopungua 20, wanadaiwa kuumia vibaya baada ya kuangukiwa na bango wakati mchezo kati ya Stevo na FC Twete unaendelea huko Uholanzi.

Tukio lilitokea nyuma ya goli wakati mchezo wa kirafiki wa Twete na Stevo jana Jumamoasi Juni 22, hali iliyozua taharuki na kusababisha hadi Helkopta za uokoaji kuwasili ili kutoa msaada.

Baada ya tukio hilo mwamuzi alisimamisha mchezo ambao baadae ulighairishwa na baadhi ya wachezaji walisogea eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada.

Baadhi ya mashabiki walioepuka kudhurika katika ajali hiyo walionekana wakitembea huku wakiwa wamechanganyikiwa.

Mbaya zaidi kabla ya mchezo kulikuwa na fataki zilizotoa moshi mwekundu zilizowashwa na mashabiki na baada ya tukio hilo, moshi huo ulisababisha kuwepo na ugumu zaidi katika uokoaji .

Mmoja kati ya mashabiki alionekana akitoka eneo la tukio huku mikono ikiwa kichwani na akilia kwa maumivu.

Baada ya helkopta ya kwanza, muda mfupi baadae iliingia nyingine ili kuzidisha nguvu ya uokoaji.

Taarifa kutoka tovuti ya Oost zilieleza kwamba hakuna aliyefariki katika majeruhi waliookolewa.

FC Twente pia ilitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ikisema wapo karibu na mashabiki waliodhurika ambao kwa sasa wanaendelea vizuri.

Chanzo: Mwanaspoti