Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bango la bao 5 za Simba; Yanga wapo sahihi - Mchambuzi

Yanga Bango Bango la bao 5 za Simba; Yanga wapo sahihi - Mchambuzi

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia Kipenga Extra ya East Africa Radio, Martin Mwakiposa amesema kuwa kitendo cha Klabu ya Yanga kuweka bango barabarani kuwazodoa wapinzani wao Simba Sc ni sahihi kwani ni sehemu ya kuwapa furaha mashabiki zao.

Mkunda amesema hayo baada ya Yanga kuweka bango barabarani linaloonyesha mabao 5-1 waliyowafunga wapinzani wao Simba, Novemba 5, 2023.

"Mimi siwalaumu Yanga kuweka lile bango, kwa sababu imepita takribani miaka 13 ndio tunaona tukio kama hili la mtu kufungwa goli 5. Kwa hiyo Yanga wanachofanya ni kuwafurahisha mashabiki zao.

"Na njia mojawapo ya kuwafurahisha ni kuweka bango ambalo atakayepita akiwa kwenye upande wa goli 5 itaendelea kutoa tabasamu, lakini atakayekuwa kwenye upande wa goli 1 itazidi kumkera," amesema Martin Mwakiposa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: