Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangala usajili mpya Dodoma Jiji, atambulishwa rasmi

Bangala Pic Randy Bangala

Thu, 7 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dodoma Jiji ni mwendo wa kutoa wachezaji nje ya nchi, baada ya Ghana sasa ni zamu ya DRC Congo.

Uongozi wa klabu hiyo umemtambulisha rasmi mshambuliaji Randy Bangala ambaye ni mdogo wake na kiungo wa Yanga Yannick Bangala kuitumikia timu hiyo msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC.

Tayari Klabu hiyo imeshawatangaza wachezaji wawili raia wa Ghana ambao msimu uliopita waliichezea Biashara United.

Mapema leo Klabu hiyo ilimtambulisha kiungo ambaye hucheza dimba la chini ama la juu Christain Zigar na jana ilimtambulisha Collins Opare ambaye hucheza Striker.

Randy hucheza nafasi ya ushambuliaji mara ya mwisho aliichezea timu ya TP Les Croyant ya DRC Congo na amewahi kuzichezea timu za Fc Renaissance,Jeunesse Sporting Tsangu na AS Maniema Union za DRC Congo.

Striker huyo anaenda kuimarisha sehemu ya ushambuliaji ya timu hiyo kufuatia Anuary Jabir kujiunga na Kagera Sugar.

Miongoni mwa majina ambayo yanatajwa kusajiliwa na timu hiyo na wanaosubiri kutangazwa ni Jimmy Shoji kutoka Mbeya Kwanza, Amaan Kyata kutoka Coastal Union, Hassan Mwaterema kutoka Kagera Sugar na wengineo ambao majina yao wamefichwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live