Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangala apata majanga Azam FC

Dg Bangala Fei Toto Yanick Bangala na Feitoto mazoezini.

Sat, 5 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa tulizozipata kutoka ndani ya Klabu ya Azam ni zinaeleza kuwa kiungo wao mpya, Yanick Litombo Bangala amepatwa na majeraha wakati akiwa kwenye mazoezi na timu yake hiyo.

Inaelezwa kwamba, kutokana na majeraha hayo, Bangala anaweza kuwakosa waajiri wake za zamani Yanga Sc katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Mkwakwani Tanga.

Ikumbukwe kiwa, Yanga na Azam FC wanatarajiwa kukutana Jumatano, Agosti 9, 2023, zikiwa zimesalia siku nne pekee.

Bangala amejiunga na Azam FC hivi karibuni akitokea Yanga mara baada ya ya Wananchi kumuuza kwa wauza Ukwaju hao wa Mbagala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live