Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangala aomba ulinzi

Bangala Tuzoo Yannick Bangala

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Ameshindwa kuvumilia. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya nyota na kiraka wa Yanga, Yannick Bangala kuwageukia marefa wa Ligi Kuu Bara akitaka wampe ulinzi uwanjani kutokana na kuchezewa rafu mara kwa mara nyingine za hatari zinazoweza kumsababisha majeraha makubwa.

Bangala alisema sio yeye pekee hata wachezaji wengine wenye majina wamekuwa wakichezewa ovyo na wachezaji wa timu pinzani, bila wahusika kuchukuliwa hatua, jambo alililosema linachangia wacheza rafu kuendelea kufanya hivyo na kwenda kinyume na mbiu ya Cheza Kiungwana!

Akizungumza nyota huyo anayemudu kucheza kama beki na kiungo alisema hataki kuwaangilia waamuzi, lakini wanapaswa kuwalinda wachezaji wawapo mchezoni ili waweze kutimiza malengo yao kisoka huku akikiri anaitegemea miguu yake kujiingizia kipato hivyo lazima alindwe.

Bangala amefunguka hayo saa chache tu tangu aliponusurika kuvunjwa mguu na Juma Ntenje wa Coastal Union katika mechi ya Ligi Kuu Bara lililopigwa juzi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na kuhamaki kiasi cha kujikuta wote wawili wakilimwa kadi za njano na mwamuzi Raphael Ikambi.

“Nawaomba sana waamuzi wawalinde wachezaji ili kuwaepusha na majeraha yasiyo na ulazima, kwani yeye ni mmoja ya wachezajui ambao wamekuwa wakifanyiwa rafu mara kwa mara, bila waamuzi kuchukua hatua kali kukomesha uhuni uwanjani,” anasema Bangala na kuongeza;

“Nimefanyiwa tukio baya sana katika mechi ya juzi, nikiri nilichokifanya pale nilipohamaji ni kosa, lakini mwili ulikuwa umeshachemka na nimefanyiwa kitendo ambacho nilitarajia mwamuzi atatoa adhabu kwa mchezaji husika hajafanya hivyo mchezo wa soka ni burudani na kazi tusifikie mahala kuharibiana karia zetu.”

Bangala alifafanua kwa kusema; “Tukio nililofanyiwa kila mmoja ameona na sio mara ya kwanza kufanyiwa ukatili kama huo mimi sio muongeaji ni mtendaji uwanjani kwa kucheza, lakini imefika mahali natakiwa kujitetea ili nisikilizwe kilio changu nahitaji kucheza zaidi mpira ndio ajira yangu tucheze mpira mambo mengine hayana maana zaidi ni kumuondoa mtu kwenye kazi anayoitegemea.”

“Ukifanyiwa madhambi na mchezaji mmoja na refa akashindwa kuchukua hatua naweza akarudia tena makosa yeye mwenyewe au mchezaji mwingine anarudia makosa aliyoyafanya mwenzake hakuna mchezaji anapenda kuumia.”

WASIKIE WADAU

Mwamuzi wa zamani aliyeombwa kuhifadhiwa jina, alisema ili kuzuia matukio yasiyokuwa ya kiungwana ni kutoa adhabu kwa wachezaji kwa kuwaonyesha kadi zilizoelekezwa kwenye shria za soka.

“Nimeshuhudia matukio yote mawili yanastahili kadi nyekundu na nimatukio ambayo waamuzi wote walikuwa kwenye nafasi nzuri za kuona sijafahamu ni kwanini walishindwa kutoa adhabu kwa wahusika kuacha kufanya hivyo ni kutishia amani kwa wachezaji kuwa nahofu wanapokuwa viwanjani,” alisema mwamuzi huyo ambaye hakutaka jina lake litaje.

Wakati huohuo mwamuzi mwingine wa zamani ambaye pia hakutka jina lake liandikwe gazetini alisema wachezaji wote walionyesha dhamira mbaya kwa mchezaji husika walistahili kuonyeshwa kadi nyekundu huku akikisi kuwa na wao ni binadamu wanapitiwa hivyo wanahitaji umakini zaidi ili kuwalinda wachezaji.

“Kuna ubinadamu pia na wao wanamapungufu lakini matukio yote mawili kati ya Henock Inonga na Salum Abubakar na Yanick Bangala ambaye alionyeshwa kadi ya njano kutokana na kulipa ubaya kwa ubaya kikanuni sio sahihi hivyo kuonyeshwa kadi ya njano alistahili.”

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz