Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangala ana rekodi zake Mbeya

Bangala 58309 Yannick Bangala

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya msimu huu 2022/2023 kumalizika kiungo wa Yanga, Yannick Bangala kutochukua tuzo zilizoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lakini ameweka rekodi ya aina yake kwa kuzifunga timu za Mbeya.

Yanga msimu huu ilipoteza michezo miwili ya ligi dhidi ya Simba 2-0 na Ihefu FC kwa mabao 2-1, ambapo katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Higlands Mbarali Mkoani Mbeya dakika ya nane ya mchezo, Bangala aliandika bao kwa kichwa huku Lenny Kissu na Never Tigere wakiipatia ushindi Ihefu.

Katika mchezo huo, Bangala alisimama kama beki wa kati kabla ya nafasi hiyo kuchukuliwa na Ibrahim Bacca ambaye amekuwa na muendelezo mzuri.

Mchezo wa kumaliza msimu ambao pia Yanga walikabidhiwa kombe lao, Fiston Mayele alivunja mwiko wa kutoifunga TZ Prisons baada ya kufunga bao moja sambamba na Bangala aliyefunga bao la pili kwa aina ileile ya kichwa na kuifanya timu hiyo kumaliza msimu kwa ushindi wa mabao 2-0, ugenini.

Msimu wa mwaka 2021/2022, Bangala alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu, hata hivyo msimu huu amefanikiwa zaidi baada ya kuchukua tuzo tatu ndani ya wiki moja.

Chanzo: Mwanaspoti