Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bangala amtikisa Mzazi Yanga

Bangala 58309 Bangala amtikisa Mzazi Yanga

Tue, 25 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yanga juzi ilitambulisha kikosi kipya cha msimu ujao, bila nyota watatu walioibeba timu hiyo msimu uliopita akiwamo Yannick Bangala, jambo lililomshtua kocha wa zamani wa timu hiyo, Kennedy Mwaisabula 'Mzazi' aliyeutaka uongozi uanike kilichowafanya wamteme kiungo huyo.

Mbali na Bangala, Yanga haikumtambulisha Djuma Shaban na straika Fiston Mayele inayeelezwa anakaribia kuuzwa Pyramids ya Misri, lakinio kukosekana kwa kiungo huyo kuliibua mijadala mtandaoni na kumfanya Mzazi ashindwe kujizuia na kuliambia Mwanaspoti ameshtushwa mno.

Mzazi alisema, japo mchezaji kuachwa ni jambo la kawaida na pia hawezi kuhoji juu ya Djuma au Mayele, lakini kwa Bangala anapata kigugumizi kuamini kama Yanga imemtema kiungo huyo aliyes ajiliwa misimu miwili iliyopita kutoka FAR Rabat ya Morocco na kuongezewa mkataba mpya.

"Bangala alikuwa MVP msimu uliopita ni kiungo bora sana, sasa kuondoka kwake Yanga sijaelewa kakutwa na nini viongozi watuambie wanayanga tujue kitu ili tuondoe sintofahamu iliyopo," alisema Mwaisabula aliyewahi kuzinoa timu za Villa Squad, Cargo na Bandari Mtwara na kuongeza;

"Bangala alikuwa kiungo muhimu sana, lakini msimu huu amekuwa akionekana mara chache sana uwanjani akianzia sana benchi, kutomuona jana niliumia sana najiuliza maswali yasiyokuwa na majibu."

Mwaisabula alisema Bangala sura yake ilikuwa ikiongea akionekana kutokuwa na furaha usoni kwake, lakini ni lazima uongozi useme sababu ya kuachana naye kwani imekuwa ghafla mno.

Kuhusu Mayele alisema kwa alivyong'ara na uhitaji wake kikosini hakustahili kuondoka wakati huu lakini kwa kuwa maisha ni lazima yaendelee hakukuwa na namna kutokana na dili alizopata nje.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: