Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Banda kusukuma namba ya Miquissone Simba

Peter Banda 2?fit=1080%2C719&ssl=1 Mchezaji Mpya wa Simba, Peter Banda

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Katika kile kinachoashiria safari ya Luis Miquissone kujiunga na Al Ahly ya Misri imeiva, winga mpya wa Simba, Peter Banda amepewa jezi namba 11 ambayo ilikuwa ikitumiwa na nyota huyo kutoka Msumbiji.

Kwenye mazoezi yake ya kwanza ambayo Simba imeyafanya huko Morocco leo ambako imeweka kambi ya kujiandaa na msimu, Banda ameonekana akiwa amevaa jezi namba 11 ambayo hutumiwa na Miquissone.

Kitendo hicho kinazidi kukoleza taarifa za Miquissone kujiunga na Al Ahly inayodaiwa imekamilisha uhamisho wake kwa ada ya Dola 1 milioni za Kimarekani.

Miquissone hayupo katika kikosi cha Simba kilichoelekea Morocco kwa kambi ya maandalizi na inatajwa kuwa hajajumuishwa ili apate fursa ya kwenda Misri kukamilisha uhamisho wake.

Banda alisajiliwa na Simba, Agosti 3 akitokea Nyasa Big Bullets ya Malawi ingawa alicheza kwa mkopo katika timu ya Sheriff Tiraspol ya Moldova msimu uliopita

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz