Winga hatari kutoka Malawi, Peter Panda, amefunguka kuwa, wiki ijayo anatarajia kurudi rasmi dimbani wiki ijayo.
Nyota huyo wa Simba SC, amefunguka hayo alipokuwa kwenye mazoezi ya pamoja na wenzake baada ya kuwa nje kwa takriban miezi mitatu tangu apate majeraha Novemba 9, 2022 katika mchezo dhidi ya Singida Big Stars.
"Niko fiti siwezi kusema asilimia mia lakini ni kama asilimia sabini hivi," alisema Banda alipokuwa akihojiwa na Simba APP.
Banda aliseme, mchezo wa wiki hii wa Azam Federation watakaocheza dhidi ya Coastal Union hawezi kuwa sehemu ya kikosi lakini ana imani wiki ijayo atakuwa tayari kuipambania Simba SC.