Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Banda aishukuru Baroka

Wed, 31 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Aliyekuwa mchezaji kiraka wa Baroka FC, Abdi Banda amewashukuru wachezaji wenzake, mashabiki na benchi la ufundi la klabu hiyo baada ya kufanya nao kazi.

Banda ameachana na klabu hiyo na kusajiliwa na Highlands Park FC baada ya kuitumikia kwa miaka miwili.

"Nawashukuru wachezaji wenzangu kipindi chote nilichofanya nao kazi, viongozi pamoja na mashabiki, kupanda na kushuka kwetu hadi kufikia hapa,"alisema Banda.             

Banda lisema walikuwa katika kipindi kizuri na kigumu mpaka wamefika hapo walipo sasa.

Banda ameondoka Baroka FC ambayo ilimaliza msimu wa Ligi Kuu Afrika Kusini inayochezwa na klabu 16, ikiwa nafasi ya 14 na ilisalia baada ya kucheza mechi ya mtoano. Highlands Park FC imemaliza msimu huo ikiwa ya saba.

Hadi anatua Baroka FC awali, Banda alizichezea klabu za Coastal Union na Simba za Tanzania.

Pia Soma

 

S: Beki Abdi Banda ameaga Baroka FC ya Afrika Kusini na amewashukuru wachezaji wenzake, viongozi na mashabiki baada ya kuitumikia kwa miaka miwili.

Chanzo: mwananchi.co.tz