Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Banda: Sijawahi kupoteza mchezo kwa Mkapa

Abdi Banda 1140x640 Abdi Banda

Mon, 19 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlinzi wa Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Abdi Banda amekiri kufurahishwa kurejea tena kwenye kikosi hicho baada ya kukosekana kwa muda mrefu.

Banda ambaye anacheza soka la kulipwa katika Klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini amesema muda wote yupo tayari kuitumikia timu ya taifa pale atakapohitajika.

“Mimi sio mchezaji wa kusema lazima niitwe timu ya taifa, ninaitwa timu ya taifa kama labda mwalimu ananihitaji kama mwalimu hanihitaji basi sioni ulazima wa kuitwa”, amesema Banda.

Nyota huyo wa Zamani wa Simba anajivunia rekodi za kipekee akiwa na kikosi cha Taifa Stars na anatamani kuendelea kuzilinda rekodi hizo.

“Kitu ambacho ninafurahi ni kwamba sijawahi kupoteza mchezo katika uwanja wa Benjamin Mkapa, hii ni rekodi yangu” amesema Banda.

Abdi banda alijumuishwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger na kutanguliza mguu mmoja kwenye michuano ya mataifa ya Afrika ‘Afcon’ itakayofanyika mwakani nchini Ivory coast.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live