Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Banda: Pale kati mtihani kidogo

Abdi Banda 1140x640 Abdi Banda

Wed, 21 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Chippa United na timu ya taifa, Taifa Stars, Abdi Banda amesema mbali na majeraha na kutoitwa timu ya taifa muda mrefu lakini Kocha Mkuu wa kikosi hicho ameona kitu kutoka kwake.

Banda aliitumikia Stars kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika juzi walipopata ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza Banda alisema pamoja na kukosekana kwenye timu ya Taifa kwa muda mrefu, lakini anaamini kuna kitu cha tofauti kocha wa timu hiyo Adel Amrouche amekiona kwake.

Alisema hakuitwa muda mrefu, sababu kubwa ikiwa ni majeraha lakini kwa sasa yupo fiti kulitumikia taifa lake.

Beki huyo wa zamani wa Simba alisema kutokana na kuzoea kucheza nafasi mbalimbali Kocha huyo alimpa nafasi ya kucheza kama kiungo ambayo ni muda mrefu hakucheza kwa karibu miaka saba lakini bado alionyesha kiwango kikubwa na Stars kuibuka na ushindi.

"Wakati tumeingia kambini kocha aliniita na kunitaka nicheze namba sita na kwa upande wangu ilikuwa mechi ngumu kwakuwa sijacheza nafasi hiyo zaidi ya miaka saba na kwa uwezo wa Mungu nilifanya vizuri na tukaibuka washindi lakini naamini mechi ijayo pia tutafanya vyema.

"Sijawahi kupoteza mechi kwenye Uwanja wa Mkapa, nafikiri hii pia inaonyesha kuwa nina bahati na Taifa Stars" alisema Banda.

Beki huyo ambaye aliwahi kuitumikia Coastal Union (2012-2014), Simba (2014-2017) na Mtibwa Sugar ni mzoefu pia wa Ligi ya Afrika Kusini na kabla ya kujiunga na Chippa United (2022) aliwahi kuzichezea Baroka (2017- 2019), kisha Highland Park (2019/20).

Chanzo: Mwanaspoti