Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balozi wa Uingereza afanya ziara Yanga

F9xbSw6XsAAT7eX.jpeg Balozi wa Uingereza afanya ziara Yanga

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Balozi wa Uingereza, David Concar amefanya ziara katika ofisi za Yanga zilizopo Salamander Tower leo mchana.

Concar amewasili katika ofisi hizo saa 8:4 mchana na kusalimiana na baadhi ya viongozi kisha akakaribishwa na Rais wa Yanga, Hersi Said na kuingia nae ofisini kwake.

Uongozi wa Yanga ulioongozwa na Hersi wameingia ofisini kwa pamoja na kufanya mazungumzo yaliyotumia dakika 17 na kutoka saa 8:21.

Baada ya kikao hicho viongozi wa Yanga sambamba na balozi Concar kwa pamoja walitoka na kuendelea kumuonyesha baadhi ya ofisi zingine katika jengo hilo.

Walirejea saa 15:00 na ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe alianza kuwatambulisha viongozi wote kisha alimkaribisha Ofisa Mtendaji mkuu, Andre Mtine ambaye hakuwa na maneno zaidi ya kumkaribisha Rais wao Hesri Said.

Hersi alipokaribishwa alianza kwa kuinadi klabu yao mbele ya balozi huyo juu ya mafanikio waliyopata.

Hersi amesema wao ndio Mabingwa wa Ligi Kuu kwa mara mbili mfululizo na walifika hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita na sasa wanataka kufanya makubwa kwenye Ligi ya Mabingwa.

“Tupo kwenye hatua ya makundi hadi sasa na malengo yetu Balozi ni kuhakikisha tunapata mafanikio mengine upande huu;

“Pia tuna mabadiliko kwenye uendeshaji wetu (transformation) ambayo tayari tumeshamuonyesha,” amesema Hersi.

Hersi amesema hadi sasa bado hawajajua ni maeneo gani ambayo wataenda kushirikiana kwa pamoja.

Upande wa Balozi wa Uingereza, David Concar amesema lengo kubwa ni kuangalia uwekezaji unaofanywa kwenye soka la Afrika.

Balozi huyo amesema kwenye Ligi ya Uingereza wameona watu wengi wa Afrika wanaenda na kufanya mambo makubwa jambo linalofanya wawekeze nguvu chini huku.

“Afrika ni Bara ambalo lina wachezaji wengi na kuna nchi ambazo bado zinaendelea kwahiyo tupo hapa kuangalia tunaendelezaje soka kiujumla,” amesema Concar.

Baada ya kuzungumza na Waandishi wa habari, Hersi na Concar waliondoka kwa msafara kwenda katika mazoezi ya timu yanayofanyika Avic Town, Kigamboni.

Balozi Concar leo ametembelea timu za Simba na Yanga kwa nyakati tofauti.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: