Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balozi Amina akingiwa kifua, kuongeza muda kamati maalum Soka la Kenya

Balozi AMINA Balozi Amina

Tue, 23 Aug 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Huku baadhi ya matawi ya Shirikisho la Soka nchini (FKF) yakitishia kuelekea mahakamani baada ya Kamati ya Mpito kuongezwa muda,hatimaye uamuzi huo umepata sapoti.

Rais wa zamani wa FKF, Sam Nyamweya na Katibu Mkuu wa zamani wa CECAFA, Nicholas Musonye, wamekingia uamuzi wa Waziri wa Michezo, Balozi Amina Mohamed, kurefusha muda wa kamati hiyo.

FKF Management Committee iliyobuniwa na takriban matawi 20 ya FKF ilitaka ipewe mamlaka ya kusimamia soka baada ya muda wa awali wa FKF Transition Committee kumalizika Agosti 12, 2022.

Lakini Waziri Balozi Amina aliwapuuza na kuongeza muda wa kuhudumu wa kamati ya FKF ambayo sasa itaendelea na usimamizi wa msimu mpya wa ligi kuu.

Na huku FKF Management Commitee ikisema itaelekea mahakamani ikisisitiza kuwa hatua ya Balozi Amina haikuwa halali, Musonye na Nyamweya wametia kauli.

“Alichokifanya Balozi Amina ni kuhakikisha hakukosekani uongozi. Kurefusha muda wa Kamati ya Mpito FKF kutaipa Serikali mpya muda wa kutosha kujipanga kuchukua usukani,” alisema Musonye.

Kwa upande wake Nyamweya, alisema uamuzi huo ni mwafaka kwasababu umesaidia kuepusha mgogoro wa uongozi sababu kama Serikali haingechukua hatua hiyo basi kungezuka makundi kadhaa yaking’ang’ania usukani kila moja ikidai kuwa ndio inapaswa kuwa na mamlaka hayo.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz