Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balotelli amtaja kocha Klopp

Jurgen Klopp Mario Balotelli Liverpool 717226 Balotelli amtaja kocha Klopp

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Iwe unapenda au hupendi, maisha ya Mario Balotelli hayajawahi kukosa vituko.

Umri wake ni miaka 34, straika huyo Mtaliano bado anacheza na sasa yupo Uturuki kwenye klabu ya Adana Demirspor.

Alipokuwa England, maisha yake yanakumbukwa zaidi kwa vituko vyake alipokuwa Manchester City, ambako alifanikiwa pia kunasa taji la Ligi Kuu England katika msimu wa 2011/12.

Kuna mambo mengi ikiwamo kupigwa faini ya kukatwa mshahara wa wiki mbili alipokuwa Man City kutokana na utovu wa nidhamu. Aligombana na wachezaji wenzake, wakati mwingine alifanya hivyo kwenye mechi. Tukio lake la nje ya uwanja ni wakati zimamoto walipoitwa nyumbani kwake baada ya kuamua kuchoma moto pazia zake.

Aliondoka Man City mwaka 2013 kurudi Milan – safari hii akijiunga na AC badala ya klabu yake ya zamani ya Inter – ilionekana kama nyakati zake za kucheza kwenye soka la England zimefika tamati. Agosti 2014, Balotelli alirejea Ligi Kuu England, wakati Liverpool, kipindi hicho ilipokuwa na Brendan Rodgers, ilimsajili kwenda kuchukua nafasi ya mchezaji mwingine mtata, Luis Suarez, aliyetimkia Barcelona.

Uhamisho wake wa Liverpool haukuwa poa, alifunga mabao manne tu kwa msimu mzima kabla ya kuhamia kwa mkopo AC Milan. Aliporejea Anfield majira ya kiangazi 2016, Jurgen Klopp ndiye alikuwa kocha wa miamba hiyo na wawili hao hawakuwa na uhusiano mzuri.

Kwa mujibu wa Balotelli, wawili hao walikuwa na mazungumzo kabla hajaondoka kwenye timu hiyo. Straika Balotelli alisema: “Klopp hakuwa ananifahamu. Nilizungumza naye mara moja, aliniambia niende kwingine nikapambane huko, kisha nitarudi. Nikaondoka na hatukuonana tena.”

Badala ya kurudi Milan, Balotelli alikwenda kujiunga na Nice ya Ligue 1. Akizungumza maisha yake ya Liverpool na AC Milan, Balotelli alisema hapaswi lawama yoyote, aliposema: “Halikuwa kosa la yeyote. Mazingira hayakuwa mazuri kwangu. Sikufanya makosa yoyote kwenye mechi au kwenye mambo yangu ya nje ya uwanja, lakini niliumia na hicho si kitu kilichokuwa ndani ya uwezo wangu.”

Chanzo: Mwanaspoti