Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balinya afunguka mazito Yanga

94393 Balinya+pic Balinya afunguka mazito Yanga

Wed, 5 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

BAADA ya kushindwa kuwika akiwa na Yanga, Juma Balinya ameanza kuhesabu mabao akiwa na kikosi cha Gor Mahia, inayoshiriki Ligi Kuu Kenya (KPL) baada ya kupachika mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Nzoia Sugar.

Baada ya mchezo huo wa kwanza kwake katika ligi hiyo, mshambuliaji huyo wa Uganda alizungumza na mwandishi wa Mwanaspoti na kusema muda utaongea kuthibitisha ubora na umuhimu wake kikosini.

Alifunga bao la kwanza katika dakika ya 45 na la pili dakika ya 56 huku bao la tatu likifungwa na Kenneth Muguna dakika ya 67.

Balinya alisajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa msimu huu lakini alishindwa kuonyesha uwezo wake uwanjani akifunga mabao mawili tu hivyo uongozi wa timu hiyo kuamua kuvunja mkataba wake katika dirisha dogo la usajili. Alirejea kwao Uganda na baadaye akajiunga na Gor Mahia.

Akizungumzia matokeo hayo, Balinya ambaye hakupata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Yanga licha ya kusajili akiwa mfungaji bora wa Uganda alisema anaamini ana kipaji na uwezo na alikuwa anashangazwa kukosa nafasi alipokuwa na kikosi hicho cha Jangwani.

“…Nikiwa Tanzania nilikuwa mzito kila ninapokuwa katika nafasi nzuri ya kufunga lakini huwezi kuamini huku nimepata nafasi ya kucheza mchezo wa kwanza tu tangu nimejiunga na hii timu na nimeonyesha kile nilichonacho …ninachoweza kukiweka wazi ni kwamba nipo fiti na nikiendelea kupewa nafasi, nitafanya mambo makubwa zaidi kwani napenda kufunga na ndio kazi yangu, basi nitafunga sanaa,” alisema.

Pia Soma

Advertisement
Balinya alisema anafurahia maisha ya Kenya kwani anaona malengo yake ya kupachika mabao mengi na kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita iko wazi endapo ataendelea kupata nafasi na kupewa ushirikiano na wachezaji wenzake.

Alisema licha ya kutumia muda mchache kufanya mazoezi tangu alipojiunga na timu hiyo, kocha amemwamini na kumpa nafasi hivyo hataki kuona anapoteza namba na atapambana ili kumdhihirishia hakukosea kumpa nafasi.

“Hakuna kitu kizuri kwenye soka kama kuaminiwa na kupewa nafasi, naamini katika kujituma hivyo nitapambania hilo kuhakikisha simwangushi aliyenipa nafasi, nitafanya hivyo kuhakikisha naendelea kupata nafasi,” alisema Balinya.

AMTAJA ZAHERA

Alisema akiwa Yanga, Kocha Mwinyi Zahera hakumpa nafasi ya kucheza kwa kuwa alikuwa hajui uwezo wake.

“Zahera pia alichangia kuonekana sina ninachokifanya kikosini kwa sababu alikuwa hanipi nafasi kabisa na aliniambia kuwa siendani na mfumo wake. Juhudi zangu zote hazikuwa na maana kikosini hadi walipoamua kuvunja mkataba wangu. Namshukuru Mungu naendelea vizuri huku niliko nafurahia maisha ya huku tofauti na nilivyokuwa kwenye timu ambayo sikuwa na uhakika wa namba kikosini,” alisema Balinya ambaye alisajiliwa na Yanga akiwa mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Uganda.

Chanzo: mwananchi.co.tz