Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke kachukua Ufalme wa Phiri Simba SC

Baleke X Phiri Baleke kachukua Ufalme wa Phiri Simba SC

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuna kipindi cha nyuma niliwahi kuwaambia mashabiki wa Simba sehemu fulani kuwa siku simba ikipata natural no 9(Namba 9 asilia) na akaingia kwenye mfumo vizuri basi Phiri atakaa benchi.

Ilikuwa ngumu kunielewa sababu Phiri alikuwa moto ila ndicho nilichagua kuamini. Kwa nini?

Kinachomfanya Phiri apate tabu kwenye soka letu ni kuwa muda mwingi anacheza kama play maker (mchezeshaji) na si finisher.

Soka letu la Tanzania linahitaji no 9 awe finisher zaidi kuliko kuwa play maker, yaani wewe uwe mkali kwenye kuweka mpira wavuni. Ndio maana Mayele anasemwa mchoyo ila anaufalme wake Yanga sababu anaweka Mpira wavuni.

Baleke anasemwa hana dribbling ability kubwa ila hajali yeye kila akiaminiwa na kocha anaweka Mpira wavuni ndio maana taratibu ameanza kujenga ufalme mpya kabisa pale simba.

Kama Baleke hatachuja basi inaweza kuwa mwisho wa zama nzuri za Moses Phiri pale Simba.

Imeandikwa na John Mchambuzi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live