Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke hamfikii Maxi Nzengeli - Mchambuzi

Maxi Nzengeli X Baleke Baleke hamfikii Maxi Nzengeli - Mchambuzi

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kutoka East Africa Radio, Samwel Rashid maarufu kama Wakanda Republic amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Maxi Nzengeli ni bora kuliko mshambuliaji wa Simba SC, Jean Baleke.

Wakanda amesema hayo baada ya Maxi kumbwaga Mkongomani mwenzake Jean Baleke na Aziz Ki na kufanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu iliyotangazwa jana na Bodi ya Ligi.

"Baleke mechi ya Mtibwa alifunga lakini mwisho wa siku unakuja kuangalia kwamba namna ambavyo alikuwa ana-perform ile work-rate yake uwanjani hauwezi ukalinganisha na alichokuwa anakitoa Max kwenye hizi mechi mbili alizozicheza kwenye kikosi cha Yanga," amesema Samwel Rashid.

Maxi amesajiliwa msimu huu na Yanga akitokea Manyema FC ya nyumbani kwao Congo DR na kuonyesha kiwango bora katika mechi chache za Ligi na Kimataifa ambazo ameshacheza mpaka sasa ndani ya kikosi hicho cha Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu kinachonolewa na Miguel gamondi.

Maxi Nzengeli

-Mechi 2

-Mabao 2

-Assist 1

Jean Baleke

-Mechi 2

-Mabao 2

-Assist 0

-Kadi ya njano 1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live