Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke awafunika Jobe na Fred

Baleke 592526 Baleke awafunika Jobe na Fred

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati kocha wa Simba, Abdelhak Benchikha akipanga kusaka nyota mpya wa kumaliza tatizo la ufungaji, aliyekuwa straika wa timu hiyo, Jean Baleke mambo yanaendelea kunyooka Libya akifunga mabao matatu katika mechi tano akiwafunika Pa Jobe na Freddy Michael walirithi wake Msimbazi.

Baleke anayekipiga Al lttihad ya Libya ametupia mabao hayo yakiwa sawa na yote yaliyofungwa na warithi wake Simba.

Nyota huyo aliondoka Simba katika dirisha dogo la usajili baada ya mkataba wake wa mwaka mmoja kumalizika akiwa tayari ametupia mabao manane.

Kutokana na kuondoka kwake, Simba iliingia sokoni na kunasa saini za Pa Omar Jobe na Freddy Michael ambao hadi sasa bado hawajathibitisha kama ni bora zaidi ya walioondoka yaani Baleke na Moses Phiri.

Licha ya Baleke kuondoka akiwa amecheza mechi chache akitupia mabao manane, wawili hao wameshindwa kufikia idadi ya mabao aliyoacha lakini pia wameshindwa kufikia rekodi aliyoiandika Libya.

Baleke akiwa na Al lttihad amecheza mechi tano kati ya hizo ameingia kambani mara tatu wakati Feddy akiwa na Simba tangu amefunga mabao mawili huku Jobe akifunga moja.

Freddy mabao yake alifunga dhidi ya Singida Fountain Gate timu yake ikishinda mabao 3-1, pia 2-1 dhidi ya Coastal Union wakati Jobe bao lake alifunga dhidi ya Tabora United wakishinda 4-0.

Simba imebakiza mechi 11 kumaliza msimu swali ni je? wawili hao wanaweza kuvunja rekodi kwa kufunga mabao manane kila mmoja.

WASIKIE WADAU

Kocha wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Boniface Mkwasa amesema uamuzi uliofanywa na Simba kuwaacha wachezaji wawili kwa wakati mmoja ni kujitoa mhanga kwani wamevunja muunganiko ambao tayari ulitengenezwa na sasa wanaanza upya.

“Siwezi kuzungumzia zaidi ishu yao kwani ni makubaliano ya pande mbili kuvunja mkataba na klabu ndio inayoajiri, lakini kiufundi wamevuruga ushirikiano uliokuwepo awali ambao ulionekana kuanza kuzaa matunda sababu ni kukosa muunganiko licha ya kutengeneza nafasi nyingi.

“Timu haijengwi kwa siku au saa, inahitaji muda ili kuwa na ushirikiano, lakini suala la kuondoa na kuleta wengine ni kutoa kazi nyingine ya kuhakikisha wanatengeneza kikosi cha muunganiko mpya. Sina shaka lakini hofu ni kama watashindwa kuwika kwa wakati husika,” amesema.

Kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema Simba ina kocha bora na mwenye rekodi nzuri ya kutwaa mataji Afrika, kama uamuzi wa kuachana na washambuliaji hao kaufanya naungana naye kwa asilimia 100, lakini kama ni viongozi wamekosea.

“Viongozi kuamua kuacha mchezaji ambaye yupo kwenye mahitaji ya kocha ni kosa kubwa kwani wanakuwa wanaingilia kazi ya benchi la ufundi, lakini kama ni uamuzi wa kocha ambaye ana uwezo  mkubwa kunizidi mimi sina budi kuungana naye,” alisema Julio, kocha wa zamani wa Taifa Stars. Simba inakamata nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live