Mon, 26 Feb 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Jean Othos Baleke ameendelea kuchana nyavu akiwa na uzi wa Al Ittihad Tripoli huko Libya.
Baleke ambaye ni raia wa Congo DR, juzi alifunga mchezo wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya nchini humo dhidi ya Asaria.
Baleke aliondoka Simba wakati wa dirisha dogo la usajili msimu huu akiwa na mabao 8 kwenye Ligi Kuu ya NBC.
Ndani ya mechi mbili pale Al Ittihad Tripoli kafunga mabao mawili, jambo ambalo linamfanya sasa ajihakikishie namba kwenye kikosi cha Kocha Thomas Mark Friedrich Mohr ambacho kinaongoza Ligi katika Kundi B.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live