Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke achimba mkwara Horoya

Jean Baleke MTIBWA 1140x640 Baleke

Sat, 18 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Simba, Jean Baleke amesema kazi kubwa imefanywa na viongozi, benchi la ufundi na sasa kilichobaki ni wao kuonyesha thamani yao wakati watakapoikabili Horoya leo Jumamosi.

Timu hizo zinakutana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa huku Simba ikihitaji ushindi utakaowafanya kufikisha pointi tisa na kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza nasi jijini Dar es Salaam, Baleke alisema wao kama wachezaji wanatambua jinsi gani mchezo huo una umuhimu kwao hivyo wako tayari kupambana kwa ajili ya mashabiki zao.

"Tumekuwa na wakati mzuri wa maandalizi na kilichobaki ni kuonyesha kile ambacho mashabiki wetu wanakitarajia kutoka kwetu, ni mchezo mgumu sana ila tunaamini tuna uwezo wa kupata ushindi."

Baleke aliongeza moja ya jambo kubwa linalompa matumaini ya kushinda mchezo huo ni kutokana na utayari na uthubutu wao kama wachezaji kwa sababu wamekuwa wakihimizana mara kwa mara kikosini.

"Kila muda tumekuwa pamoja na tukizungumzia mchezo huo tu sasa hii inaonyesha ni kwa jinsi gani tunahitaji kufanya mambo makubwa yatakayotupa heshima lakini kuwafurahisha mashabiki zetu pia."

Wakati Baleke mzuka ukiwa mwingi hali ni tofauti kwa wageni wao kwani kiungo mshambuliaji wa Horoya, Seyei Sebe Baffour ameingiwa na hofu huku akidai ni ngumu kushinda ardhi ya ugenini.

"Ni ngumu sana kucheza ugenini tena katika mazingira haya lakini tutajaribu ili kupata matokeo mazuri, wenzetu wameshinda michezo miwili iliyopita hivyo tunategemea mchezo mzuri na mgumu."

Baffour aliongeza Simba ina faida tofauti na wao hususani linapokuja suala mashabiki ambao kwa kiasi kikubwa anaamini watajitokeza kwa wingi kuwapa sapoti ingawa na wao hawatoingia kinyonge.

Simba iko nafasi ya pili na pointi sita huku Raja Casablanca iliyokuwa ya kwanza kufuzu kwenye kundi hilo ina 12, Horoya iko ya tatu na pointi nne wakati Vipers iko mkiani na pointi moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live