Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baleke, Robertinho wapokea tuzo zao Mbarali

AC0A24CE 14D7 4AF5 B07C C1A20564D9F3.jpeg Straika wa Simba , Jean Baleke akipokea tuzo yake ya Mchezaji Bora Mwezi Machi

Mon, 10 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Straika Jean Baleke, kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveria 'Robertinho' na Meneja wa uwanja wa Highland Estate, Malule Omary wamekabidhiwa tuzo zao za mwezi Machi baada ya kufanya vizuri katika nafasi zao.

Baleke aliibuka mchezaji bora ligi kuu wa mwezi huo akiwashinda wenzake Jeremiah Juma na Daruwesh Saliboko alioingia nao kwenye kinyang'anyiro.

Kwa upande wake Robertinho aliwashinda Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredin Nabi na Abdalah Mohamed 'Bares'.

Naye Meneja Omary alochaguliwa na kamati ya tuzo kufuatia kuweka vizuri miundombinu ya uwanja. Tuzo hizo zimetolewa leo kwenye uwanja wa Highland Estate Mbarali wakati Simba na Ihefu zikijiandaa kuingia uwanani kucheza mchezo wao wa ligi kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live