Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bale kuukosa mchezo dhidi ya Ubelgiji

Gareth Bale Gareth Bale

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Winga wa Wales, Gareth Bale hatakuwepo kwenye kikosi cha Wales kitakacho menyena na timu ya taifa ya Ubelgiji kwenye mchezo wa kufuzu kombe la Dunia siku ya jumanne.

Gareth Bale ambaye siku ya jumamosi alikuwa anasherekea mchezo wake wa mia moja(100) kuichezea timu yake ya taifa ya Wales, ambapo alicheza kwa dakika 45, baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na majeruhi.

Gareth leo jumatatu amejitenga na timu na kufanya mazoezi peke yake, shirikisho la mpira wa miguu nchini Wales baadae watatoa tamko rasmi kama Bale atakuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kwenye benchi katika mchezo dhidi ya Ubelgiji au hatokuwepo kabisa.

Kikosi cha Robert Page kinahitaji angalau alama moja tu kwenye mchezo wa jumanne ili wajihakikishie nafasi ya pili kwenye kundi E ili wapate nafasi ya kwenda kucheza play off.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live