Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bale atoa matumaini Real Madrid

Bale Gareth Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale akiwa mazoezini leo

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hali ya majeruhi ya Real Madrid inaendelea kuimarika, huku Gareth Bale akirejea mazoezini.

Los Blancos walikuwa na changamoto ya majeruhi mapema msimu huu wakiwa wameanza vibaya msimu kutokana na majeraha.

Lakini mambo yameimarika sana katika wiki za hivi karibuni, na kufuatia kurejea kwa Fede Valverde, sasa inaonekana kama chezaji mwingine muhimu amerudi.

Gareth Bale alifanya mazoezi kwenye nyasi siku ya Alhamisi na alifanya mazoezi na kikosi leo Ijumaa

Inatarajiwa Gareth bado ataikosa gemu ya wikiendi hii dhidi ya Real Sociedad, huku Real Madrid wakitarajia kuwa makini na kumtumia staa huyu kutokana na rekodi ya hivi majuzi ya afya ya raia wa wales.

Bale alirejea mapema kuichezea Wales wiki chache zilizopita na akapata jeraha jingine.

Staa huyu anaweza kupatikana kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa wiki ijayo dhidi ya Inter Milan, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kucheza na Atletico Madrid wikendi ifuatayo.

Ingawa, sasa ana kibarua kigumu kupata nafasi ya kuanza kutokana na fomu nzuri ya Marco Asensio na Rodrygo.

Gareth Bale amecheza mechi tatu pekee za La Liga akiwa na Real Madrid msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live