Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balama, Morrison waipa Yanga ushindi kwa Lipuli

94645 Pic+yanga Balama, Morrison waipa Yanga ushindi kwa Lipuli

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mabao ya Balama, Morrison waipa Yanga ushindi kwa Lipuli S:Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 34, katika nafasi ya tatu wakati Azam ikiwa ya pili (38) na Simba ikiendelea kuongoza kwa pointi 50. Thobias Sebastian Dar es Salaam.Yanga imeichapa Lipuli kwa mabao 2-1, huku waamuzi wasaidizi akiweka rekodi ya kutoa uamuzi tata katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara. Yanga ilipata mabao mawili katika kipindi cha kwanza kupitia kiungo Mapinduzi Balama na Benard Morrison huku bao la kufutia machozi la Lipuli likifungwa na Mwasa. Ushindi huo unaifanya Yanga kufikisha pointi 34, katika nafasi ya tatu wakati Azam ikiwa ya pili (38) na Simba ikiendelea kuongoza kwa pointi 50. Tatizo la waamuzi kushindwa kutafsiri sheria limeendela kuwa kubwa baada ya mwamuzi msaidizi kutoa uamuzi tata wa kutoa kona kwa Lipuli katika mpira aliokuwa ameudaka kipa wa Yanga, Mechata Mnata ambao ameodaka katika mwamba. Wachezaji wa Lipuli walipiga uamuzi huo wakiamini walistahili kupata bao hilo, lakini mwamuzi alitoa kadi kwao na kuamuru kona wakati kipa wa Yanga, Mnata alikuwa amedaka na mpira ulikuwa ndani ulitakiwa kuendelea. Katika mchezo huo Yanga ilitumia dakika 13, kupata bao la kuongoza baada ya Balama kuunganisha kwa kichwa cha kupiga mbizi krosi iliyopigwa na beki Juma Abdul. Baada ya kupata bao hilo Yanga waliendelea kushambulia lango la Lipuli dakika 31, winga wa Mghana Morrison aliifungia timu yake bao la pili baada ya kupiga shuti kila lililotokana na krosi ya Juma Abdul iliyoshindwa kuokolewa na mabeki wa Lipuli. Wakati Yanga wakiendelea kutakata zaidi kuliko Lipuli kwa umiliki wao wa mpira na kushambulia mara kwa mara kwa upande wa mshambuliaji Yikpe Gislan alishindwa kuonyesha ubora wake. Yikpe alikosa bao ilikuwa dakika 9, baada ya kuekewa krosi safi na Ditram Nchimbi, lakini alishindwa kumalizia. Dakika 35, alipewa tena krosi kutoka upande wa kulia wa Yanga lakini Yikpe aliimalizia na kupiga shuti ambalo lilipaa juu ya lango la Lipuli. Hakuishia hapo Yikpe dakika 37, alikosa tena bao baada ya kukutana na pasi ndani ya boksi na kupiga shuti ambalo liliokolewa. Lipuli wao walionekana kukamatika na Yanga kwani walikuwa wakitumia kupiga mipira mirefu mingi kwa mshambuliaji wao Paul Nonga. Mipira hiyo mirefu ilionekana kukosa madhara kwani walinzi wa Yanga, Lamine Moro na Juma Makapu.

Chanzo: mwananchi.co.tz