Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Balaa linalotengenezwa Simba ni la kurejesha ufalme wao

Simba Simba Simba.jpeg Balaa linalotengenezwa Simba ni la kurejesha ufalme wao

Tue, 25 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ukiambiwa Simba hawatanii, hawatanii kweli na safari yao ya usajili ndiyo imeanza hivyo kwa kushusha mastaa watatu kutoka nje na mmoja wa hapo wa hapa ndani.

Msimu ujao wa 2024/25 utakuwa mtamu kuliko unavyofikiri maana mastaa wanaoshushwa na Simba wanajua boli kweli kweli.

Msemaji wa Simba Ahmed Ally mewaweka wazi mikakati yao ikiwemo suala la usajili wa nyota wapya na kuweka wazi mastaa wanaohusishwa kusajiliwa.

Mastaa hao wenye uchu wa mataji ni kiungo mkabaji Augustine Okejepha kutoka Rivers United ya Nigeria, Elie Mpanzu kutika AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Sergie Pokou wa Asec Mimosas ya Ivory Coast wakiungana na mtoto wa nyumbani hapa hapa  Yusuph Kagoma kutoka akitokea Singida Fountain Gate.

Ahmed ameongeza kwamba mastaa hao walioonyesha viwango vikubwa walipokuwa wakizitumikia timu zao za awali na watachukua nafasi za wachezaji ambao hawakuwa na wakati mzuri ndani ya Simba.

Akizungumza nasi, Ahmed amesema usajili wa Elie Mpanzu, hawezi kusema kama wamemsajili au wapo kwenye mazungumzo, mchezaji mzuri na walimfatilia mechi yao mwisho ameona ameaga.

“Ni mchezaji mzuri anavutia kucheza Simba, kumsajili au kutomsajili kwa hilo siwezi kama viongozi wa juu wanafanya mazungumzo na nyota huyo basi muda ukifika tutaweka wazi.

Suala la Kagoma tunaheshimu mkataba wake na Singida, tunaheshimu masuala ya mkataba wa mchezaji na timu yake, kiungo mzuri ana uwezo wa kukata umeme kwa ubora alikuwa nao anauwezo wa kushika dimba Simba,” amesema Meneja huyo, Hatma ya kiungo wao, Aubin Kramo amesema ametibiwa na daktari amejiridhisha baada ya kupata vipimo kuwa yupo tayari kurejea uwanjani na atakuwa sehemu ya wachezaji ambao wataenda nchini Misri kwa ajili ya Kambi, muda kwa kufurahia uwezo wake umekaribia.

“Kuhusu kutoa ‘thank you’, zoezi linaendelea, lilisimama kwa muda kwa sababu ya wachezaji ambao tunatarajia kuwaacha bado wana mikataba tunamalizana nao kwa kuwapa stahiki zao na tutakapowatema basi tuwe huru na kuepukana na kesi za kupelekana FIFA,” amesema Ahmed.

Amesema usajili mzuri unafanywa na ikiwemo kuvunja mkataba kwa mchezaji ambaye haonekani kuwa msaada ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao uongozi utalazimika kuvunja mkataba ili kupisha mwingine kusaidia timu kufikia malengo.

“Malengo yetu msimu ujao kufanya vizuri katika mashindano ya kombe la shirikisho ikiwemo kucheza nusu au fainali, kufikia huku lazima tufanya usajili mkubwa kwa kuleta wachezaji wazuri watakaofika malengo yetu,” amesema Ahmed.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live