Wed, 23 Aug 2023
Chanzo: Tanzaniawe
Mashabiki wa Klabu ya FC Lorient juzi kwenye mchezo wa kwanza nyumbani dhidi ya Nice, waliweka mabango ambayo yalionekana kupinga uwepo wa wachezaji watatu wa timu hiyo akiwemo Benjamin Mendy ambaye amesajiliwa hivi karibuni baada ya kesi yake ya ubakaji kumalizika na kukutwa hana hatia.
Mabango hayo yalisomeka jumbe mbali mbali ikiwemo;
“Hatutaki wabakaji kwenye uwanja wetu.” wakimaanisha kuwa hawawataki wachezaji wenye tuhuma za unyanyasaji wa kingono kwenye timu yao, na wachezaji waliotajwa ni pamoja na Mendy, Achraf Hakimi na Wissam Ben Yedder.
Chanzo: Tanzaniawe