Asiyefanya kazi na asile. Ndicho ambacho Moise Katumbi Rais wa TP Mazembe ameamua kwa mastaa wake.
Wachezaji wa Kikosi cha TP Mazembe watakatwa mishahara yao kwa asilimia 25 kama wakishindwa kufuzu kutinga Robo Fainali katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kuchukuliwa kwa hatua hii sio suala la ghafla tu, ni baada ya mfululizo wa matokeo mabovu hivyo Katumbi amewaambia atalazimika kukata robo ya mishahara yao kama wakishindwa kuvuka hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mazembe wako Kundi D sambamba na Timu za Us Monastir wenye alama 7 baada ya michezo yao mitatu, Yanga nafasi ya pili na lama 4, Mazembe wana alama 3 huku wakiwa wamepigwa michezo miwili kati ya mitatu na Real Bamako alama 2 mkiani.