Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bakhresa ashauriwa kuhusu Azam FC

Yusuf Bakhresa.jpeg Bakhresa ashauriwa kuhusu Azam FC

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mmiliki wa Azam FC, Mmiliki wa timu ya Azam FC, Yusuf Bakhresa ameshauriwa kuwa timu yake isifukuze makocha kila wakati badala yake iwape muda wa kutosha ili kuijenga timu hiyo ili ifanye vizuri.

Maoni hayo yametolewa na shabiki kindakindaki wa Azam FC, Aman Robert kutoka Nduguti, Mkalama mkoani Singida ikiwa ni saa chache baada ya Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba Sc.

”Bakhresa kwa ushauri wangu kama shabiki wa Azam FC, ni kuwapa muda makocha tusiwe tunawafukuza mara kwa mara, sio kila kocha atakayekuja ni mbovu.

"Tunaweza kumpa hata Guardiola wa Man City akaja Azam FC akashindwa na kuondoka. Anatakiwa atulie aangalie ni wapi timu inafeli,” amesema Aman Robert.

Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Azam FC ilimtimua kocha wake mkuu, Denis Lavagne raia wa Ufaransa aliyedumu klabuni hapo kwa mwezi mmoja pekee. Kabla ya hapo Azam ilimtimu aliyekuwa kocha wake, Abdihamid Moallin aliyetimuliwa miezi miwili iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live