Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bakari Shime: Tunataka heshima All African Games

Bakari Shime Mchawi Mweusi Bakari Shime: Tunataka heshima All African Games

Thu, 7 Mar 2024 Chanzo: Dar24

Baada ya kuwasili salama nchini Ghana, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake chini ya miaka 20 (U-20) Tanzanite, Bakari Shime, amesema lengo lake ni kupata ushindi katika mchezo wa kwanza wa mashindano ya All-Africa Games ya mwaka 2024, dhidi Uganda ili kuongeza morali ya upambanaji kwa timu yake.

Tanzania inatarajia kushuka dimbani keshokutwa Jumamosi (Machi 09) kuvaana na Uganda ikiwa ni mechi ya kwanza ya Kundi lao, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Cape Coast Sports, nchini humo, katika mashindano hayo yanayoanza kutimua kuvumbi, Machi 8 hadi 23, mwaka huu.

Shime amesema kuwa maandalizi walishafanya wakiwa Tanzania na kazi iliyopo sasa ni kukiweka sawa kikosi chake katika mambo madogo madogo ikiwamo kuwajenga kisaikolojia wachezaji kufikia mipango ya kusaka ushindi.

Amesema Uganda wana timu nzuri, lakini anaimani na vijana wake wameshika maelekezo yake, hivyo kwenda kuyatekeleza uwanjani kwa kukabiliana vema na wapinzani wao wakianza na Uganda.

“Kama nilivyosema awali kuwa hatutaenda na historia ya mpinzani wetu, bali tuweke mipango yetu imara na kutafuta ushindi katika mechi yetu ya kwanza dhidi ya Uganda kwa ajili ya kuanza vizuri michuano hii,” amesema kocha huyo.

Ameongeza kuwa licha ya kushiriki michuano mingi na kufanya vizuri anaimani All-Africa Games ni mashindano tofauti na wanahitaji kupata alama katika kila mechi kwenye kundi lao.

Tanzanite imepangwa Kundi A, ikiwa na timu ya Uganda, Ethiopia na mwenyeji Ghana.

Mchezo wao wa kwanza Tanzania itacheza dhidi ya Uganda, na baada ya hapo Tanzanite itarudi tena uwanjani Machi 12, kuvaana na wenyeji Ghana, katika na mechi yake ya mwisho ya hatua ya makundi itakuwa Machi 15, mwaka huu, dhidi ya Ethiopia itakayopigwa Uwanja wa Elmina.

Chanzo: Dar24