Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bajeti ya Man United ni kizungumkuti

Man Uniteddddddd Bajeti ya Man United ni kizungumkuti

Fri, 24 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Inaelezwa kuwa hadi sasa Manchester United ina bajeti ya Pauni 35 mlioni itakazotumia katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi hali inayozua yaharuki kwa mashabiki wao.

Bajeti hiyo ni pesa ambazo zipo tayari kwa matumizi lakini inaonekana kuwa haitoshi na ili iongeze wamiliki wenza Ineos wamepanga kuuza kundi kubwa la wachezaji katika dirisha lijalo.

Pesa zitakazopatikana baada ya wachezaji hao kuuzwa ndio zitawapa mashetani hawa wekundu nafasi ya kutumia Pauni 400 milioni kutokana na sheria za matumizi ya pesa zilivyo.

Wachezaji wanaoonekana kuwa huenda wakaipa pesa nyingi Man United ni Mason Greenwood ambaye usajili wake unaweza kufikia Pauni 60 milioni pamoja na Murcus Rashford ingawa mwenyewe amekataa kuondoka.

Mpango wa kuwauza mastaa hawa utasaidia kubalansi vitabu vyao ambapo mahesabu yatawaruhusu kutumia walau hizo Pauni 400 milioni kwenye usajili.

Greenwood anahusishwa na Napoli pamoja na Juventus wakati Rashford alidaiwa kuwa katika rada za PSG katika dirisha la majira ya baridi,

Man United kwa muda sasa inahusishwa kutaka kuwasajili Jarrad Branthwaite, Marc Guehi, Leny Yoro, Jean-Clair Todibo na Tosin Adarabioyo kwa upande wa safu ya ulinzi na katika kushambulia Benjamin Sesko anatajwa kuwa katika orodha ya watakaosajiliwa ingawa inaweza kuwa ngumu kwani Chelsea pia inamhita

Chanzo: Mwanaspoti