Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bailly kupishana na Martinez OT

Baily Pic Data Eric Bailly

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya AC Milan imeripotiwa kuingia kwenye kinyanganyiro cha kumsajili beki wa Manchester United, Eric Bailly.

Kwa mujibu wa ripoti Bailly huenda akaondoka Man United, baada ya ujio wa Lisandro Martinez, aliyetangazwa hivi karibuni na amepewa jezi namba sita mgongoni, iliyovaliwa na Paul Pogba.

Beki huyo wa Kimataifa wa Ivory Coast anahofia nafasi yake ndani ya kikosi cha Erik ten Hag, kwani Martinez ni chaguo namba moja la kocha huyo.

Martinez, ameigharimu Mashetani Wekundu, kitita cha Pauni 55 milioni na ataungana na Harry Maguire, Raphael Varane na Victor Lindelof.

Wakati huohuo Roma imemtolea macho Bailly, huku Jose Mourinho akimtaka beki huyu kwa udi na uvumba. Ikumbukwe Bailly alisajiliwa na kocha huyo mwaka 2016 kipindi anainoa Man United, kabla ya kufukuzwa.

Lakini kwa mujibu wa Athletic, AC Milan imeingilia kati dili hilo na kutibua mipango ya Roma. Kocha wa AC Milan, Stefano Pioli ameendelea kukinoa kikosi chake baada ya kubeba ubingwa wa Serie A msimu uliopita.

Bailly si mchezaji pekee wa Ligi Kuu England anayewaniwa na AC Milan, yupo Hakim Ziyech anayekipiga Chelsea ambaye yupo huru kuondoka dirisha hili la usajili.

Chelsea imeitaka Milan kutoa kitita cha Pauni 8.4 milioni licha ya kumsajili kwa pesa ndefu ya Pauni 24.6 milioni mwaka 2020. Mazungumzo kati ya klabu hizo yalianza tangu wiki kadhaa zilizopita na hata hivyo muafaka haukuafikiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live