Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bahati mbaya kwa Djuma Shabani

Djuma Shabani WA0027 Bahati mbaya kwa Djuma Shabani

Sat, 2 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dirisha la usajili Tanzania lilifungwa juzi usiku, huku mastaa kadhaa wakisajiliwa saa chache kabla ya kufungwa, lakini bahati mbaya ikawa kwa aliyekuwa beki wa Yanga Sc, Djuma Shabani aliyekwama kutua Azam baada ya kipa Ali Ahmada aliyekuwa kwenye mipango ya kutemwa kuchomoa dakika za jioni.

Azam FC ilikuwa tayari kumsajili Djuma na alikuwa ameanza mazoezi na wakali hao Chamazi, lakini juzi ikakwama kumsajili baada ya Ahmada kugoma kuondoka.

Timu hiyo ilitaka kumtoa Ahmada ili nafasi yake aingie Djuma, lakini kipa huyo aligoma kwa kile alichohofia kukosa timu kwani madirisha mengi ya usajili yamefungwa.

Kwa maana hiyo kugoma kuondoka kwa Ahmada kuliifanya Azam kuwa na wachezaji 12 wa kigeni kama kanuni inavyotaka.

Kutokana na hali hiyo licha ya Djuma kufanya mazoezi na timu hiyo kwa sasa atalazimika kusubiri hadi dirisha dogo litakalofunguliwa katikati ya Disemba hadi Januari mwakani ili apate timu ya kuchezea.

Baada ya mambo kuwa magumu, Azam kupitia kwa msemaji wao Zakazakazi wakasema hawakuwa na mpango wa kumsajili Djuma kwani wao walikuwa wameshafunga usajili wao kitambo kabla ya dirisha kufungwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live