Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Bado wachezaji wanakosa umakini"- Pablo

Pablo Frano Arrows Kocha Mkuu wa Simba Pablo Franco Martin

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuingoza Simba na kuibuka na ushindi wa magoli 3-0 katika dimba la Mkapa Dar es Salaam, Kocha wa Wekundu wa Msimbazi akiri wana mapungufu makubwa kutoka katika kikosi chake.

Akizungyumza mara baada ya mchezo wa leo Pablo amesema;

"Nina furaha lakini sio sana kwa sababu bado tuna mchezo mwingine ugenini. Tumecheza vizuri lakni bado sijaridhika sana na umakini wa wachezaji wangu"

"Kwa hali ilivyokuwa, namna timu ilivyoimarika na namna kila mmoja anavyopambana naweza kusema nimefurahi, lakini sio sana sababu bado tuna mchezo wa ugenini ambao tutakutana na timu ngumu.” amesisitiza Pablo

Simba iatasafiri kuwafuata Red Arrows mchezo utakaopigwa Disemba 5, huko nchini Zambia.

Simba inatafuta nafasi ya kufuzu kwa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live