Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bado tuna safari ndefu kufikia levo za Al Ahly - Try Again

Bado Tuna Safari Ndefu Kufikia Levo Za Al Ahly   Try Again Bado tuna safari ndefu kufikia levo za Al Ahly - Try Again

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, Salum Abdallah 'Try Again' amesema kama klabu na Taifa la Tanzania, bado kuna safari ndefu ya kufikia mafanikio katika soka.

Try Again ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano maalum na Azam TV akielezea masuala mbalimbali ikiwemo zawadi ya mashabiki bora waliyoipata kwenye mashindano ya African Football League (AFL).

"Tau (Percy) analipwa dola laki nane kwa mwaka, aliyekuwa anacheza naye Tshabalala labda ni ten parcent ya hiyo kwa mshahara wake kwa mwaka, unaweza kuona tofauti ya madaraja. Kipa yule wa Al Ahly analipwa takriban dola elfu hamsini, sitini na kuendelea.

"Kipa wetu aliocheza nafikiri mshahara wake na signing fees zake zote haziwezi kuzidi dola elfu mbili au elfu tatu kwa mwezi. Tuanayo safari ndefu ya kufikia mafanikio hatua kwa hatua," alisema Try Again.

"Mamelodi wana wachezaji Chile, Brazil dola Miloni tatu, Milioni mbili sisi dola Milioni moja ni usajili wa timu nzima kwa mwaka, kwa hiyo huwzei kwenda mbinguni kabla hujafa, lazima tukubali kwamba tunahitaji kufanya kazi, tunahitaji kuwekeza zaidi," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live