Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bado saa chache tu kipigwe Mzizima Dabi

Arajiga Awafuata Bado saa chache tu kipigwe Mzizima Dabi

Thu, 9 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda ni kuanzia saa 12:15 jioni ambapo mtanange huo utaanza. Ni mechi ya kukata na shoka katika Ligi Kuu. Mechi inayojulikana kwa umaarufu wa jina la ‘Mzizima Dabi’. Ni mechi dume haswa.

Mechi iliyobeba matumaini ya timu zote mbili kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu ujao lakini pia ni mechi ya kuamua ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Mwamuzi wa pembeni ni kutoka Sudan Ibrahim Abdallah atakayeshika kibendera kama mwamuzi msaidizi namba moja huku msaidizi namba mbili akiwa Mohamed Mkono kutoka Tanga huku Mwanadada Amina Kyando kutoka Morogoro akiwa mwamuzi wa nne na katikati ya uwanja mwamuzi mkuu atakuwa Ahmed Arajiga kutokea Manyara ambaye mara nyingi amekuwa akichezesha mechi kubwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live