Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bado nyie!kwani mmejiandaaje?

Simba Now (600 X 750) Simba inakutana na Yanga Disemba 11

Mon, 6 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bado nyie, kwani mmejiandaaje? ndio swali ama kauli ambayo Simba SC kuwaelekea wananchi hivi sasa baada ya kaumalizana na mtanange wao dhidi ya Red Arrows ya ZambiaSiku ya Jumapili, Disemba 5.

Simba walisafiri mpaka Lusaka nchini Zambia kwa minajili ya kwenda kusaka tiketi ya kufuzu kwa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Katika mchezo huo wa upinzani, Simba ilipoteza kwa magoli 2-1 lakini wanafuzu hatua inayofuata kwa ushindi wa jumla wa magoli 4-2, baada ya kupata ushindi katika mechi ya awali wa magoli 3-0 Novemba 28 kwa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa ratiba baada ya Simba kumalizana na mchezo huo, mechi inayofuata ni dhidi ya mtani wa Jadi Yanga, Ligi Kuu ya NBC.

Pengine morali waliyoipata Simba kutoka katika mchezo dhidi ya Wazambia ndio inayowapa hamasa ya kuitaka Yanga muda wowote hivi sasa.

Kumbu kumbu ya mchezo wa mwisho baina ya miamba hii miwili ni Septemba 25 mwaka huu katika mchezo wa ngao ya Jamii, ambako mnyama Simba alikubali kichapo cha bao 1-0, bao lililowekwa wavuni na Fiston Mayele.

Simba watakuwa wenyeji wa Yanga, Disemba 11 katika uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live