Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bacca ana siri nzito

Bacca Out Leo Bacca ana siri nzito

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa Yanga na Taifa Stars anayewindwa na madalali kadhaa barani Ulaya na Afrika, Ibrahim Hamad 'Bacca' amefichua siri nzito kuhusu kiwango chake na kitu ambacho hatakisahau Afcon 2023.

Stars iliyokuwa ikishiriki kwa mara ya tatu katika fainali hizo za Afcon ilimaliza na pointi mbili katika kundi F, huku Bacca akiwa miongoni mwa mastaa waliong'ara.

Bacca aliyecheza mechi zote tatu, amefichua kwamba hawezi kuisahau mechi dhidi ya Morocco ambayo walilala mabao 3-0. Amesema kwamba alipambana kibabe, lakini mastaa wa timu hiyo walikuwa hawazuiliki na walikuwa wanashambulia kwa mbinu nyingi.

Bacca amesema mechi hizo zimemuongezea uwezo mkubwa wa kimbinu, kwani alicheza na wachezaji wenye uzoefu zaidi yake na atakuja na utofauti mkubwa kwenye ligi na michuano mingine ambayo Yanga inashiriki.

"Nimecheza na wachezaji wanaocheza ligi kubwa nchi za Ulaya na kazi ya yangu kubwa ilikuwa ni kuzuia na kila nilipokuwa naingia uwanjani akili yangu ilikuwa inawaza kufuzu tu ndio maana nilifanya kila niwezalo.

"Sasa narudi nikiwa nimekuwa kiakili,kifikra na ukubwa wangu umeongezeka kwani nimekutana na watu waliojuu zaidi yangu na wamenikubali," amesema Bacca na kuongeza; "Ninaporejea Yanga mimi sio yule wa mwanzo, naiona nafasi yangu kuwa kubwa zaidi, kwani nimekuza ubora wangu hivyo nimezidi kuwa fiti na mwenye uzoefu."

Stars watarejea hivi karibuni na wachezaji kuingia vikosi mwao kama kawaida ili kuendelea na mechi za mashindano ya Ligi ya Mabingwa bila kusahau Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho (ASFC).

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: