Beki wa kati wa Yanga Ibrahim Abdullah ‘Bacca’ amesema anafurahi kucheza na mabeki wote waliopo Yanga kutokana na kila mmoja kuwa na aina yake ya uchezaji huku akisisitiza kuwa anafurahi zaidi akicheza na Bangala kama namba sita.
“Mabeki wote nimepata nafasi ya kucheza nao wana uwezo na ni viongozi wazuri kiwanjani lakini nafurahi zaidi nikicheza na beki mwingine kati na Bangala akawa juu kama namba sita ni mtu makini sana na anapenda kuzungumza mimi namuita beki kiongozi;
“Mkicheza uwanjani kwa kukumbushana majukumu mchezo wa mpira ni mwepesi na makosa mengi yanapungua tuna nahodha Mwamnyeto anazungumza ana kila sifa ya kuwa kiongozi lakini kuna Bangala hapendi timu ifungwe kizembe.” alisema.