Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bacca: Tupo tayari kuwapa burudani Wananchi kesho

Bacca 1024x1024 Bacca: Tupo tayari kuwapa burudani Wananchi kesho

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuelekea siku ya Party la Kibingwa ambapo Yanga watacheza mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United, wachezaji wamesema wapo tayari baada ya kufanya maandalizi ya kutosha.

Kesho Jumamosi kuna Party la Kibingwa pale Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga watakapokabidhiwa ubingwa wa Ligi Kuu ya NBC baada ya mchezo dhidi ya Tabora United.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, Ibrahim Bacca amesema: “Wachezaji tumejiandaa vizuri sana, tumeshafanya mazoezi ya kutosha kutoa burudani kwa wachezaji.

Najua mashabiki wetu wanajua baada ya mchezo kutakuwa na burudani ya kutosha hivyo watajitokeza kwa wingi.

“Nitashangaa kama kuna shabiki wa Yanga hatafika uwanjani hapo kesho. Matukio kama haya ni matukio ambayo yanatokea mara chache na mashabiki wanajua wapi tulipotoka. Wachezaji tupo tayari kazi imebaki kwenu wananchi kujitojeza kwa wingi.

“Haijalishi ni nani atapewa nafasi ya kucheza, sisi wenyewe tunaaminiana, tunafahamu kila mchezaji aliyepo Yanga ana mchango mkubwa kwa klabu yake. Kwa maana hiyo kila mchezaji atakayepata nafasi basi ataonesha kile bora alicho nacho.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live