Beki wa Yanga SC, Ibrahim Bacca amewatumia ujumbe mashabiki wake wa Zanzibar baada ya kubeba Ubingwa mbele ya Azam FC huku akisema hajawaangusha mashabiki zake nyumbani na kazi aliyoifanya wameiona Uwanjani.
Bacca kwenye mkutano na Waandishi wa Habari alisema wakati Abdul Suleiman "Sopu" hakuwa anapata nafasi kwenye kikosi cha Yanga SC lakini alitumia nafasi ya kumtazama na aliifanyia kazi mikimbio yake yote akiwa Uwanjani.
“Niwashukuru Wananchi waliojitokeza kutusapoti lakini hawakuniangusha kuja kwao kwa wingi, hapa ni nyumbani. Mpira ni furaha na sikuwaangusha watu wa nyumbani, nadhani kazi wameiona,” amesema Bacca.