Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bacca: Msimu ujaio Ihefu tutawapiga kote kote

Bacca Ihefu Bacca: Msimu ujaio Ihefu tutawapiga kote kote

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati wa Kikosi cha Yanga, Ibrahim Hamad Bacca amesema kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC watahakikisha wanamfunga Ihefu nyumbani na ugenini ili kumfunga kabisa mdomo baada ya kuwasumbua kwa misimu miwili.

Bacca amesema hayo baada ya kumaliza deni lao na timu ya Ihefu FC ambapo jana Jumatatu, Machi 11, 2024, waliifunga mabao 5-0 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi.

“Nilisema kisasi ni haki kwa sababu Ihefu walitufunga kwao na sisi tukavumilia kwa muda mrefu, lakini leo nadhani Wananchi wameona, haki yetu imelipa na sasa hivi roho ziko safi na hatuna deni tena na Ihefu.

“Ninataka nitoe angalizo kwamba, panapo uhai na majaliwa, msimu ujao tutamalizana na Ihefu kote kote, nyumbani na ugenini, hakuna tena mambo ya kisasi ni kote kote tutawapiga nje ndani,” amesema Bacca.

Itakumbukwa kuwa, Ihefu ndiyo timu iliyofungwa na Yanga bao 2-1 msimu uliopita na kuiharibu unbeaten yao ya 49 kuelekea 50.

Msimu huu, Ihefu ndiyo timu pekee ambayo imeifunga Yanga kwenye michezo yake yote 18 ambayo imecheza, hivyo Wananchi walikuwa na kila sababu ya kulipa kisasi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: