Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bacca: Mama yangu anamkubali Job

Job Na Bacca 681x437 Bacca: Mama yangu anamkubali Job

Thu, 9 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki kisiki wa Yanga, Ibrahim Abdullah 'Bacca' amesema mama yake ambaye ni shabiki mkubwa wa Simba, anavutiwa na aina ya uchezaji wa beki wa kati na nahodha msaidizi wa Yanga, Dickson Job.

Bacca alisema hayo jana baada ya kutamatika kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC ambao Yanga iliondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar mfungaji akiwa Mudathir Yahya dakika ya 82.

Beki huyo wa zamani wa KMKM alisema Job ni mchezaji anayejitoa uwanjani na kwa kushirikiana pamoja wametengeneza ukuta imara ndani ya kikosi cha Yanga.

"Kwakweli Job ni mtu anayejitoa sana, kila mtu anaona nadhani mama yangu mzazi amewahi kumzungumzia sana akisema ni mchezaji anayemvutia sana," alisema Bacca.

Yanga imefikisha pointi 68 katika michezo 26 iliyocheza hivyo ikihitaji pointi tano tu ili kufikisha 73 ambazo hazitafikiwa na timu yoyote ambazo zitaipa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya tatu mfululizo.

Kwenye mechi 10 za mwisho ilizocheza Yanga msimu huu mabeki hao wawili Job na Bacca wameruhusu bao moja tu dhidi ya Simba Aprili 20, mwaka huu huku wakiambulia clean sheet tisa.

Yanga 0-0 Mamelodi Sundowns

Mamelodi Sundowns 0-0 Yanga

Dodoma Jiji 0-2 Yanga

Singida Fountain Gate 0-3 Yanga

Yanga 2-1 Simba SC

JKT Tanzania 0-0 Yanga

Yanga 1-0 Coastal Union

Yanga 3-0 Tabora United

Mashujaa FC 0-1 Yanga

Yanga 1-0 Kagera Sugar

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: